Thursday, February 27, 2014

Facebook kuinunua WhatsApp kwa dola bilioni 19

Posted by BongoHeadline Editor Posted on 12:33 PM with No comments
Kampuni ya Facebook Inc. imekubali kuinunua kampuni ya WhatsApp Inc. kwa dola bilioni 19. Manunuzi hayo ni makubwa zaidi kuwahi kufanyika kwenye masuala ya internet tangu muongo mmoja uliopita
Manunuzi hayo yanajumuisha dola bilioni 12 katika stock, dola bilioni 4 za cash na share zenye thamani ya dola bilioni 3. Inamaanisa kuwa waanzilishi wa app hiyo pamoja na waajiriwa watapewa stock ya dola bilioni 3 itakayodumu kwa zaidi ya miaka minne tangu mkataba huo. Mwanzilishi mwenza wa kampuni hiyo, Jan Koum atajiunga na bodi ya Facebook.
Jan Koum
Mkataba huo unawafanya waanzilishi wa WhatsApp, Jan Koum na Brian Acton wawe mabilionea. Facebook inasema itaicha WhatsApp kama huduma inayojitegemea kama ilivyofanya kwenye Instagram.
Ni biashara kubwa zaidi ya internet kuwahi kufanyika toka Time Warner ilipoungana na AOL, mwaka 2001 kwa thamani ya dola bilioni 124. WhatsApp ina zaidi ya watumiaji milioni 450 na kila siku watumiaji milioni 1 wapya wanaongezeka.
Mark Zuckerberg: WhatsApp is the only app we’ve ever seen that has grown more quickly than Facebook itself
Mark Zuckerberg, CEO wa Facebook
Mwenyekiti Mtendaji wa Facebook, Mark Zuckerberg, aliyeununua mtandao wa Instagram kwa dola milioni 700 mwaka 2012, amekuwa akiongeza applications za ujumbe na habari kwa watumiaji wa smartphonena tablet. WhatsApp, itakayokuwa mali yake ya kujivunia, itakuwa ikichuana na Twitter na Snapchat.